Fr. Denis Massawe (CPPS) ni Mmisionari wa Shirika la Damu Takatifu ya Yesu aliyehudumu katika Parokia ya Mt. Gaspari del Buffalo – Mbezi Beach kama Paroko Msaidizi na Msimamizi wa Kituo cha Hija. Amehudumu katika Parokia ya Mt. Gaspari kwa takribani miaka 7, kuanzia mwaka 2019 hadi 2026, ambapo sasa anatumwa kuendelea na utume wake Roma nchini Italia.
Pichani ni Wanaparokia wa Parokia aliyohudumu, wakimpongeza kwa utume uliotukuka na kumtakia heri na baraka kwa utume wake mpya.