Matangazo Ya Jumapili 1 November
-
Leo ni Dominika ya SHEREHE YA WATAKATIFU WOTE
-
Dominika ijayo ni Dominika ya 32 ya mwaka A wa Kanisa
USAFI na usimamizi ni zamu ya JNNK zifuatazo:
1. MISA YA KWANZA Mt. Vicent 2. MISA YA PILI Mt. Theresia wa Mtoto Yesu 3 MISA YA TATU Mt. Joseph Mfanyakazi 4 MISA YA NNE Ushirika wa Moyo Mt. wa Yesu Telezesha pembeni kuona jedwali lote -
Tunawashukuru wote waliofanya USAFI Jana Jumamosi na kutoa huduma kanisani Mt. Margaretha Maria waliku 08,Bikira Maria Mama wa Damu Azizi ya Yesu walikuwa 12 na Mt. Yuda Thadei walikuwa 09 Jumuiya zote walitoa mchango wa mapambo, Mwenyezi Mungu awabariki nyote Kwa majitoleo yenu.
-
Kesho Jumatatu,ni Siku ya kuwaombea marehemu wote Misa zitakuwa Tano, Saa 12, Saa 1:00, saa sita mchana, saa 9 alasiri na saa 11 Jioni. Waamini wote tufike kuwaombea Wapendwa Marehemu wetu tufike tukiwa na Mishumaa midogo.
-
Waamini wote waliopata Sakrament ya Kipaimara hapa Parokiani kuanzia mwaka 2008 hadi 2019 mnaombwa mfike ofisini kwa sista kukamilisha kujaza taarifa zenu .
-
Karismatiki Katoliki wameandaa Maombi ya siku 07 yatakayoongozwa na Fr. Mapinduzi kuanzia Jumapili ijayo tarehe 08.11.2026 hadi 15.11.2026 muda ni saa 9 hadi saa 12 Jioni.
-
Masista wa Mashirika ambayo wanahudumu hapa Parokiani wanawashukuru waamini wote kutoka kila Jumuiya kwa mapaji mliyoyatoa kwa ajili ya kuwategemeza katika nyumba zao Mwenyezi Mungu awabariki kila mmoja wenu kwa moyo wenu wa upendo
-
Uongozi wa Radio Maria Tanzania unawakumbusha waamini ambao hawajarudisha Bahasha za Kapu la Mama yetu Bikira Maria wazipeleke ofisini kwa sista, Dominika ijayo tutasoma kila Jumuiya Bahasha walizopewa na Bahasha walizorudisha
-
Makusanyo ya Wiki: (Yasomwe)
-
Matangazo ya ndoa: (Yasomwe Kama yapo)