JUMAPILI YA YESU KRISTU MFALME
Maelezo Zaidi
C:Yesu Kristo ni Mfalme wa kweli Mwishoni mwa mwaka wa kiliturujia, tunamtafakari tena Kristo Yesu Mfalme, aliyetoa maisha yake, akateseka, akasulubiwa na kufa msalabani kwa ajili yetu. Yeye ni mfalme wa mbingu na dunia, enzi na utawala wote ni wake. Nasi tukimfuata kwa uaminifu, mwisho wa maisha yetu hapa duniani ukifika, atatukaribishe katika ufalme wake mbinguni. Na Padre Paschal Ighondo –Vatican. Tafakari ya Neno la Mungu, dominika ya 34 mwaka C wa kiliturujia katika Kanisa, kipindi cha kawaida. Ni dominika ya mwisho ya mwaka C wa kiliturujia. Dominika ijayo ni ya kwanza ya majilio, mwaka A. Katika dominika hii ya mwisho, kiliturujia tunaadhimisha Sherehe ya Bwana wetu Yesu Kristo Mfalme. Licha ya kuwa katika Dominika ya Matawi tulifanya maandamano, tukikumbuka jinsi Yesu Kristo alivyoingia Yerusalemu kwa shangwe kama Mfalme, umati mkubwa wa watu ulivyomlaki, wakishika matawi mikononi na kumshangilia. Mwishoni mwa mwaka wa kiliturujia, tunamtafakari tena Kristo Yesu Mfalme, aliyetoa maisha yake, akateseka, akasulubiwa na kufa msalabani kwa ajili yetu. Yeye ni mfalme wa mbingu na dunia, enzi na utawala wote ni wake. Nasi tukimfuata kwa uaminifu, mwisho wa maisha yetu hapa duniani ukifika, atatukaribishe katika ufalme wake mbinguni. Ni katika muktadha huu wimbo wa mwanzo unasema hivi; “Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima. Utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele” (Ufu. 5:12, 1:6). Ni katika tumaini hili mama Kanisa katika sala ya mwanzo anasali; “Ee Mungu Mwenyezi wa milele, umependa kutengeneza upya mambo yote katika Mwanao mpenzi, Mfalme wa ulimwengu. Utujalie kwa wema wako, viumbe vyote vilivyokombolewa utumwani, vikutumikie na kukusifu bila mwisho