ASKOFU MKUU KATIKA MISA YA KUMBUKIZI YA MISA YA MAUAJI YA UCHAGUZI
Maelezo Zaidi
Taifa letu limepoteza heshima kutokana na yale yaliyojiri wiki ya uchaguzui mkuu.Sio tu limepoteza heshima,lakini imepoteza watu ambao wameuwawa kiholelea.Katika masimulizi,wako watu waliouwawa wakiandamana,lakini adhabu ya kuandamana sio kifo cha risasi.Wako watu waliouawa majumbani mwao.Ni katika tafakari ya Askofu Mkuu Ruwa'ichi wakati wa Misa ya kuombea majeruhi na marehemu waliopoteza maisha wakati wa Uchaguzi Mkuu Okt,29.Pia Jimbo Kuu la Mbeya lilifanyika Misa. Na Angella Rwezaula – Vatican. Katika kile kilichojitokeza katika uchaguzi mkuu nchini Tanzania, ambapo Uchaguzi Mkuu uliopelekea maandamano na matokeo yakawa ya kupoteza maisha ya binadamu na wengine kujeruhiwa, Makanisa mbambali Katoliki nchini Tanzania yanaendelea kuwaombea marehemu wote, waliojeruhiwa na ndugu zao waliokumbwa na mkasa mbaya huo. Ni katika muktadha huo ambapo kama ilivyokuwa umetolwa mwaliko kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar- Ess Salaam, Tanzania, kwa mapadre, watawa, waamini walei, kusali, kutoka kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu hilo, Mwashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, aliongoza ibada ya misa Takatifu, Dominika tarehe 9 Novemba 2025 kwa ajili ya kuwaombea ndugu, jamaa, marafiki na raia waliouawa.